Skip to content

Kusitisha mashambulizi— kulinda haki za albino

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ambaye ameteuliwa hivi majuzi ametoa mpango wa kulinda haki za mazeruzeru. English

Published:

“Mazeruzeru wanawindwa barani Afrika!” Vichwa vya habari kama hivi vimekuwa vya kawaida siku hizi. Vichwa hivi vya habari vinaleta mihemko mikubwa lakini kwa kweli vinaangazia uhalisia hakiki: kwamba katika baadhi ya nchi, mazeruzeru wanashambuliwa -  kwa kawaida na mapanga na visu - kwa lengo la kupata viungo vya miili yao. Mashambulizi haya yana misingi yanayotokana na imani  ya ushirikina  ambamo inaaminika ya kwamba viungo fulani vya miili ya mazeruzeru vinaweza kuleta utajiri na bahati nzuri vinapotumiwa katika madawa ya wachawi. Jambo hili basi limesababisha uuzaji na ununuzi wa viungo vya mwili katika soko nyeusi, na hata, wakati mwingine, kumekuwa visa vya wizi katika makaburi ya maalbino au mazeruzeru. Viungo vya mwili vimeeripotiwa kuuzwa kwa mamia au maelfu ya dola za Marekani. Hakika, kama ni umaskini unaowafanya watu kuwashambulia wenzao ambao wako tofauti kwa sababu ya ulemavu wao wa ngozi, basi bei hizi za juu za sehemu hizi za mwili inaashiria kuwepo na ushirika wa watu wenye uwezo wa kifedha katika jamii.

Uzeruzeru ni hali ya maumbile ambayo husababishwa na upungufu mkubwa au kutokuwepo kwa melanin katika ngozi, nywele na macho. Kuna aina mbalimbali za ulemavu wa ngozi lakini ule unayojulikana zaidi - na ambao umesababishwa wale wenye uzeruzeru kuvamiwa - ni wakati ngozi yote, nywele zote na macho yote yameathirika kiwango cha kumfanya mtu aonekane tofauti katika familia na jamii yake. Ni lazima mama na baba wabebe jeni ya uzeruzeru ilikuweza kupitisha jeni hii kwa mtoto. Inaweza kurithiwa hata wakati wazazi wote wawili hawana hali hiyo. Katika hali hiyo, kuna asilimia 25 katika kila mimba ya kwamba mtoto atakuwa na uzeruzeru. Uzeruzeru kwa ujumla husababisha uharibifu wa maono kwa viwango tofauti katika kila mtu binafsi. Pia husababisha uathirikaji wa nguvu wa kupata kansa ya ngozi ambapo tahadhari ni duni au haipatikani kabisa. Idadi ya marudio ya uzeruzeru  inatofautiana kwa kanda huku Amerika ya Kaskazini na Ulaya kuwa na takribani  ya1 kati ya 17,000 walioathirika. Katika maeneo kadhaa ya Afrika kusini mwa Sahara, idadi ya marudio inaweza kuwa ya juu kama 1 kati ya 1,500. Hapa ndipo pia eneo ambamo mashambulizi yote ya kimwili yameripotiwa hadi sasa na mashirika ya kiraia yakiripoti mashambulizi juu ya 400 katika nchi 25 katika eneo hili. Hesabu hii ya mashirika haya yalianza mwaka wa 2007. Hizi tu ni kesi zilizoripotiwa; kuna uwezekano wa idadi halisi ya mashambulizi kuwa juu ya ile iliyoripotiwa.

Katika kukabiliana na mashambulizi hayo, Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa lilipitisha maazimio kadhaa kuanzia mwaka wa 2013 hadi sasa, wakilaani mashambulizi na kuonyesha ubaguzi ambao umesababisha mashambulizi hayo. Zaidi ya hayo, mwaka wa 2013, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu 'lilipitisha azimio muhimu mwaka wa 2013 (Azimio 263) wakiorodhesha hatua ambazo mataifa yanayohusika yanapaswa kuchukua ili kulinda mazeruzeru. Hivi karibuni, mwezi wa Machi  mwaka wa 2015, Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) liliamrisha kuwepo na mamlaka ya mtaalamu huru anayeendesha kampeni,uhamasishaji,uelimishaji na uwezeshaji kuhusu haki za mazeruzeru; nilishika wadhifa huu mwezi wa Agosti 2015.